March 19, 2017
Gennady Golovkin ameonyesha anaweza baada ya kumtwanga mpinzani wake Daniel Jacobs na kuendelea kutetea ubingwa wake.

Haikuwa kazi rahisi kwa Golovkin katika pambano hilo kwenye Ukumbi wa Madison Square Garden.

Jacob anayetokea New York, Marekani alionyesha uwezo mkubwa lakini alishindwa kujizuia kulamba sakafu katika raundi ya nne.


Pamoja na kulambishwa sakafu, Jacob aliinuka na kuendelea kupambana na hadi mwisho Golovkin alionyesha ni bora zaidi kutokana na kasi kubwa na ukali wa makonde yake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV