March 19, 2017
Pamoja na kuondolewa katika michuano ya  Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha George Lwandamina amesema vijana wake wanastahili pongezi.

Yanga imeondolewa na Zanaco ya Zambia baada ya sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam na sare ya 0-0 mjini Lusaka. Wazambia hao wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini.

Lwandamina amesema waliteleza kidogo kwa kuwa walikuwa na uwezo wa kuifunga Zanaco kwao Lusaka.

"Hatukutumia nafasi nyingi tulizopata, tungeweza kupata mabao na kumaliza kazi. Lakini si sahihi kuanza kulaumu sasa kwa kuwa bado tuna michuano ya kimataifa.

"Lengo letu lilikuwa ni Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini huu ni mpira. Tunachotaka ni kujirekebisha na kuendelea zaidi kwa lengo la kufanikiwa," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV