March 19, 2017Kikosi cha Simba, kiko tayari kwa ajili ya mechi yao ya Kombe la Shirikishi dhidi ya Madini FC, leo.

Simba inaivaa Madini FC ya Arusha katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo, leo.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema itakuwa mechi ngumu lakini wako tayari.

“Hatuwajui Madini lakini tunachotaka ni kufanya vizuri na maandalizi yalikuwa mazuri hivyo tuko tayari,” alisema.


Tayari Madini wamekuwa wakijigamba kuitoa shoo Simba katika mechi hiyo huku Simba wakiendelea kusisitiza itakuwa mechi ngumu kwao. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV