March 26, 2017


Kama wewe ulikuwa unamuona hafai, kwao Chile wanamjali. Maana wameamua kutengeneza sanamu maalum la Alexis Sanchez.

Mshambuliaji huyo anayeelezwa ana mpango wa kuondoka Arsenal, ametengenezewa sanamu maalum akiwa na Kombe la ubingwa wa Copa America mwaka 2015 na kikoombe cha mchezaji bora wa michuano hiyo.


Kama haitoshi kuna nembo ya timu maarufu ya Chile, Colo Colo aliyocheza msimu mmoja kwa mkopo na nembo nyingine ni FC Barcelona na Arsenal.

Heshima yake, ndani ya Chile ni kubwa sana kama gwiji na alihudhuria uzinduzi wa sanamu lake hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV