March 20, 2017Uwezo anaouonyesha kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, umekuwa gumzo kiasi cha kuvuka mipaka na kuingia Uganda, kwani aliyewahi kuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi amedai anasikia salamu zake.

 Okwi aliachana na Simba msimu wa 2014/15, baada ya kutakiwa kujiunga na timu mpya ya Sonderajyske ya Denmark, kabla ya siku za hivi karibuni kuamua kuvunja mkataba huo na kurudi kwao Uganda kuitumikia Klabu ya Sports Club Villa.

Okwi amesema kwamba, tangu amerudi kwao Uganda amekuwa akisikia tu kuwa Simba ina mchezaji anaitwa Kichuya lakini yeye hajapata muda wa kumfuatilia na kumuona kama kweli anaitendea haki jezi namba 25 aliyokuwa akiivaa.

 “Kweli ninapata salamu za Simba inavyofanya kwa sasa na mara kadhaa namsikia huyo Kichuya akitajwa ila ukweli sijawahi kumuona akicheza, hivyo siwezi kumzungumzia  sana.

“Ujue mimi kwa sasa niko bize na timu yangu hapa Uganda, kwa hiyo muda wa kuangalia wenzangu saa nyingine nakuwa nakosa kwani nipo karibu na familia zaidi,” alisema Okwi.

SOURCE: CHAMPIONI  


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV