March 20, 2017Mkurugenzi wa Ufundi wa zamani wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amepanga kuwaonyesha uwezo wake halisi wale wote waliokuwa wakimbeza kwa kuwafunga wote atakaokutana nao, ikiwemo Yanga.

Pluijm amejiunga na Singida United baada ya uongozi wa Yanga kumpa barua kusitisha mkataba wake kwa kile walichodai timu hiyo kuyumba kiuchumi.

 Pluijm amesema kuwa anashukuru kwa kuweza kupata timu ya kufundisha nchini kwani malengo yake yalikuwa kuangalia mbele lakini kwa sasa anajipanga kuonyesha uwezo wake halisi katika ligi ya msimu ujao.

“Kiukweli namshukuru Mungu kwa sababu zimekuja ofa nyingi lakini bado nina mapenzi na soka la Tanzania, hivyo kuwepo kwangu hapa katika timu hii kuna maana kubwa sana.

“Kikubwa nataka kuwaaminisha watu ukweli  halisi kuhusu uwezo wa kazi yangu, naomba Mungu anisaidie katika kila kitu ili kufikia lengo hilo, kwani nahitaji kufanya vizuri nikiwa na timu yangu mpya kwenye ligi ya msimu ujao, bila ya kuangalia timu ipi nitakutana nayo,” alisema Pluijm. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV