March 20, 2017


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameunda kamati ya saa 24 ambayo itachunguza suala la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Cluods Media Group, usiku wa kuamkia juzi.


Makonda anatuhumiwa kuvamia studio za Clouds akitaka kipindi cha Shilawadu kurusha picha zinazomuonyesha mwanamke anayelalamika kuzaa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Uzima na Ufufuo.

Pia Makonda anatuhumiwa kuondoka na flash aliyochota kipindi kizima na kuanza kukisambaza mitandaoni.

Pamoja na Nape, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari (Moat), Reginald Mengi, naye amelaani tukio hilo na kumtaka Nape kuomba radhi.

Nape na Mengi, walijumuika na Wana Clouds Media Group, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wao, Joseph Kusaka pamoja nna Mkurugenzi wa Vipindi, Ruge Mutahaba ambaye pia alilaani kitendo hicho.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV