March 23, 2017


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewataka Watanzania kukubaliana na suala la  kusitishwa kwake uteuzi wa cheo hicho.

Rais John Magufuli amemteua Dk Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo ya Nape.

Akizungumza na waandishi nje ya Hoteli ya Protea, leo. Nape amesema wanatakiwa kukubaliana na hali halisi.

“Mkubali Tanzania ni kubwa kuliko Nape na hampaswi kuanzisha matatizo. Tanzania ni nchi yetu sisi na tujue Nape hawezi kuwa mkubwa kuliko Tanzania.


“Nawashauri kuwa watulivu, namshukuru Rais Magufuli kwa kunipa nafasi ya kufanya naye kazi kwa mwaka mzima.


“Nilifanya kazi yangu kwa akili na nguvu zangu zote. Nawashukuru wasanii, waandishi, wanamichezo kwa ushirikiano wenu. Nilipenda kuendelea kufanya kazi nanyi lakini muda wa aliyeniteua umefika, nitawakumbuka sana, ninawapenda sana,” alisema Nape.


Wakati anataka kuondoka katika eneo hilo, gari lake lilizuiwa na RPC wa Kinondoni, Suzan Kaganda hali iliyosababisha taharuki hadi Nape aliwapowaomba waandishi kuondoka eneo hilo ili naye aondoke.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV