March 2, 2017


Kocha Mkuu wa Tuvu Shooting, Malale Hamsini amesema wao ndiyo wanaopaswa kujilaumu kutokana na kufungwa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga.

Hamsini amesema walikuwa na nafasi kubwa ya kuifunga Yanga, lakini wakapoteza nafasi nyingi za kufunga huku wakipoteza umakini katika safu ya ulinzi.

Yanga iliitwanga Ruvu Shooting kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara, jana.

Wakati Yanga inashinda mechi hiyo, ilikuwa pungufu mtu mmoja kwa dakika 45 zote za kipindi cha pili baada ya Obey Chirwa kutolewa kwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

“Tulipoteza nafasi za wazi, hatukutulia licha ya kusisitiza hilo. Hakuna wa kumlaumu hapa,” alisema.

Hata hivyo, Hamsini amesema wanaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV