Kikosi cha Simba kimeweka kambi katikati ya jiji la Dar es Salaam kujiandaa na mechi yao ijayo dhidi ya Mbeya City.
Kambi ya Simba ipo Kariakoo katikati ya jiji la Dar es Salaam na imekuwa ikipiga mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi jijini Dar es Salaam.
Simba ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara, watashuka dimbani Jumamosi kuwakaribisha Mbeya City.
Simba imeingia kambini jana ikiwa ni siku chache baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani wake Yanga.
Kikosi hicho chini ya Kocha Joseph Omog kinalazimika kuendelea kushinda mechi ili kutowapa nafasi watani wao Yanga wenye pointi 52 wakati Simba wanaongoza wakiwa na 54.
0 COMMENTS:
Post a Comment