March 15, 2017


Leicester City imeweka rekodi baada ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa mara ya kwanza.

Leicester imeitwanga Sevilla ya Hispania kwa mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Wes Morgan katika dakika ya 27 na Marc Abrighton katika dakika ya 54.

Hii ni suprise nyingine katika ulimwengu wa soka baada ya Leicester kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England na kuwashangaza wengi.
Sanir Nasri wa Sevilla alilambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu katika dakika ya 74, lakini Steven Nzonzi akapoteza nafasi katika dakika ya 80 baada ya Sevilla kupata penalti lakini kipa Kasper Schumeichel kuiokoa.

Lakini haikupewa nafasi  kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini imeonyesha inaweza kwa kuitwanga Sevila kwa jumla ya mabao 3-2 na kutinga nusu fainali ikiwa ni baada ya ushindi wa 2-0, leo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV