March 5, 2017




-Msuva anaruka juu na kuunganisha krosi lakini Saidi anadaka na kuokoa, goal kick
-Friday anaingia, anaachia shuti kali hapa, nje


DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89, Wachezaji wawili wa Mtibwa Sugar wako chini hapa, ndiyo wanapatiwa matibabu
Dk 87 mpira wa kona wa Msuva, Nduda anaruka na kudaka kwa ufundi kabisa
SUB Dk 83 anatoka Mbonde anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Hussein Javu
Dk 83, Mahadhi anaingia vizuri unaokolewa na kuwa konaDk 81 Kessy anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini Mbonde anaweka kichwa na kuokoa
Dk 79, krosi safi ya Msuva, Lundenga anaokoa na kuwa kona, inachongwa na kuwa kona tena
Dk 78 Mpira unaonekana kuchangamka, lakini bado timu zinacheza mpira wa juu zaidi


Dk 77, Friday anaingia anaachia shuti kali lakini Makapu anazuia kabisa
SUB Dk 75, Kelvin Friday anaingia kuchukua nafasi ya Chanongo
SUB Dk 71, anatoka Yondani, nafasi yake ianchukuliwa na Said Juma Makapu
Dk 68, Kessy anaachia mkwaju mkali kabisa lakini anapaisha hapa
Dk 67, Yondani anafanya kazi ya ziada katikati ya uwanja kusambaza mipira
Dk 66, krosi nzuri ya Mwashiuya lakini Nduda anadaka vizuri
KADI Dk 60, Kessy analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mohamed Issa


SUB Dk 59 anaingia Geofrey Mwashiuya kuchukua nafasi ya Emmanuel Martin
Dk 58, Mtibwa wanaingia vizuri kabisa, lakini shuti la Mbonde linakuwa halina kasi
Dk 56, Mbonde anaondosha hatari baada ya krosi nzuri ya Chirwa
Dk 55, mpira unaendelea kuwa mto, Yanga wanapeleka mashambulizi mengi zaidi
Dk 52, Yanga wanapata kona, inachongwa lakini Nduda anafanyiwa madhambi
Dk 45 mpira umeanza kwa kasi inaonekana Yanga wanataka kupata bao la mapema



MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Nduda anadaka mpira lakini unamtoka, unamkuta Mahadhi anaachia mkwaju mkuuuubwaaa
Dk 42, Salim Abdallah anampiga kanzu Chirwa, anaachia shuti kali kabisa lakini goal kick
Dk 40 Dida anaruka na kuokoa mpira unakuwa kona, inachongwa lakini goal kick
Dk 37: Matokeo bado ni 0-0, mchezo umebalansi pande zote, timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dk 35: Penalti ya Msuva inapaa juu ya lango upande wa kulia.


Dk 35: MSUVA ANAKOSAAAAAAAAAAA
Dk 34: Msuva anaenda kupiga penalti hiyo.
Dk ya 33: Yanga wanapata penalti baada ya beki wa Mtibwa kuunawa mpira. 
Dk 30, Yanga wanafanya shambulizi kali langoni na Mtibwa, Chirwa anapiga lakini shuti lake linazuiwa na mabeki wa Mtibwa.
Dk 24, Chanongo anaingia vizuri ndani ya eneo la 18 lakini anaanguka mwenyewe
Dk 23 bado mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali sana
Dk 19 mpira safi wa krosi, Nditi anapiga kichwa cha kurukia, goal kick
Dk 16, Busungu anaingia vizuri na kuachia shuti kali kabisa
KADI Dk 14, Yondani analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mbonde
Dk 13, Dida anaruka vizuri na kuokoa mpira wa kona ya Baba Ubaya tena


Dk 12, Dida anafanya kazi ya ziada, anaokoa mpira wa Baba Ubaya na kuwa kona
Dk ya 9 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja zaidi, bado hakuna shambulizi kali
Dk 5, Zulu anaachia mkwaju mkali hapa, hata hivyo Said Mohamed anaudaka kwa ulainiiiii
Dk 4 krosi safi ya MSuva, lakini Mtibwa wanakuwa makini kuokoa
Dk 3, Chirwa ndani ya eneo la hatari la Mtibwa anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick
Dk 1, mechi imeanza lakini taratiiibuu kila mmoja akionekana kuusoma mchezo

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic