March 5, 2017

 

Yanga imeshindwa kufika kileleni baada ya sare ya bila mabao dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, leo.

Ilikuwa mechi yenye mvuto na Yanga watajilaumu baada ya kupata penalti dakika ya 33, lakini Simon Msuva akapiga shuti kuubwa juu ya lango la Mtibwa Sugar.

Sare hiyo, inaifanya Yanga kufikisha pointi 53 hivyo kuiacha Simba ikiendelea kutamba kileleni na pointi zake 55 baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Mbeya City, jana.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV