March 9, 2017


Kitendo cha Barcelona kufunga mabao mawili hadi mapumziko dhidi ya PSG kimezua gumzo kubwa mitandaoni.

Wako ambao wamekuwa wakijiuliza kama Barcelona wana uwezo wa kusawazisha na kuongeza mabao. Kwani mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa ugenini Paris, Ufaransa walichapwa mabao 4-0.


Mjadala ni je, Barcelona wanaweza kusawazisha mabao ypte manne na kuongeza moja? wengi wamekuwa wakiamini wanaweza. Tusubiri ngoma iishe. Hata hivyo watatakiwa kuwa makini kweli wasifungwe hata bao moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV