March 24, 2017


Ukiwa shujaa wenzetu wanakupa heshima na hiki ndicho kilichotokea kwa mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

Serikali ya kisiwa cha mji wa Madeira nchini Ureno imeamua kubadili jina la Uwanja wake wa Ndege kutoka “Madeira Airport” na kuwa Uwanja wa Ndege wa Cristiano Ronaldo.


Tayari mabadiliko yameanza kufanyika na baada ya sikh chache zijazo utatangazwa wakati wa uzinduzi rasmi.

Ronaldo ni Mreno aliyezaliwa kisiwani humo, kisiwa ambacho kilo karibu na kile cha Hispania kinachomilikiwa na Hispania Cha Tenerife ambacho Mtanzania, Farid Mussa anacheza soka hapo.


Ronaldo amekuwa nahodha wa kwanza kuiwezesha Ureno kubeba ubingwa wa Ulaya, mchezaji mwenye mafanikio akiwa England (Manchester United), Hispania na Real Madrid pia amefanikiwa kubeba ubingwa wa Ulaya na kuwa mchezaji bora wa dunia mara kadhaa.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic