Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiwa na mmoja wa wageni kutoka China.
|
Kampuni ya StarTimes Tanzania ikiungana na wasanii kutoka Tanzania na China, jana Alhamisi walizindua filamu ya kwanza ya Kichina iliyotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili iliyokwenda kwa jina la Mfalme Kima.
Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Tong Gang, naye alikuwepo.
|
Uzinduzi huo uliofanyika kwenye Viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Tong Gang.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Ole Gabriel amesema: “Kutokana na umoja unaojengwa sasa kati ya wasanii wa Tanzania na China, itasaidia sana vijana wengi kukuza tasnia yao na tamaduni wa nchi hizi mbili kwa jumla.
Wageni waalikwa pamoja na wageni wa heshima kwa pamoja wakati wa uzinduzi huo. |
“Niwaase tu wasanii wa Kitanzania kuitumia fursa hii ipasavyo ili kuitangaza vema nchi yao, lakini pia kujifunza tamaduni za wenzao na wao kuwafundisha tamaduni zetu, lengo likiwa ni moja tu kuendeleza undugu tuliokuwa nao tangu zamani.”
0 COMMENTS:
Post a Comment