March 3, 2017





Kamati ya Saa 72 ambayo inahusika kusikiliza malalamiko na mapingamizi mbalimbali yanawasilishwa na timu inatarajiwa kukutana kesho Jumamosi kupitia mambo kadhaa yaliyojitokeza kwenye ligi kuu na daraja la pili likiwemo suala la kadi ya straika wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa.

Chirwa alipewa kadi nyekundu na mwamuzi Ahmad Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Kadi hiyo ni ya kwanza kupewa Yanga kwa msimu huu.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa kamati hiyo itakutana kujadili kadi hiyo ambayo ilizua utata wa aina yake kutokana na mazingira ya alivyopewa sambamba na matukio mengine yaliyojitokeza kwenye mechi hizo.

“Kamati ya Saa 72 itakutana Jumamosi kujadili mambo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye mechi za ligi kuu ikiwemo kadi ya Obrey Chirwa wa Yanga na hata tukio la Abdi Banda wa Simba juu ya mchezaji Said Juma Makapu.

“Kama maamuzi yatafikiwa mapema basi mchezaji huyo anaweza kuwa sehemu ya mchezo kati ya timu hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumapili hii,” alisema Alfred.        



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic