March 3, 2017Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali ameibuka na kusema kuwa kitendo cha kufungwa mabao 2-1 na watani wao wa jadi Simba kimevuruga mambo mengi kwa kuwa hakutegemea lakini amesisitiza kuwa bado wana nafasi kubwa ya kuendelea kutetea ubingwa wao msimu huu.


Mzee Akilimali amesema kipigo hicho kimekuwa kikimpa wakati mgumu na hapendi kuona akikumbushwa kwani kimekuwa kikimpa maumivu makali huku akisisitiza ubingwa kwao bado haujapotea kama wanavyochukuliwa wapinzani wao.


“Unajua ule mchezo dhidi ya Simba ulikuwa ni wetu kwa sababu ushindi ulianza kuonekana mapema tu lakini mambo yakabadilika bila kutegemea na matokeo yake wao ndiyo wameibuka na ushindi, kiukweli bado naumia na wala sitaki watu wanikumbushie ile mechi kabisa.


“Ni kweli nilisema Zanzibar walitufunga kwenye bonanza sasa huku mambo yakabadilika na hali ikawa mbaya kwetu lakini niseme tu kwamba bado tupo vitani kupigania ubingwa wetu kwa sababu wapinzani wetu wametuzidi alama mbili hivi sasa, hivyo wakiteleza wamekwisha kwa kuwa huu siyo wakati wa kumtafuta mchawi,” alisema Mzee Akilimali.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV