March 11, 2017Nahodha wa Simba, Jonas Mkude, amesema wamepanga kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizobaki ili waweze kutwaa ubingwa ligi kuu msimu huu.


Simba sasa hivi ipo kileleni ikiwa na pointi 55 na nyuma yake wapo Yanga wenye alama 53 na wote wamecheza mechi 24. Simba wanahaha kuhakikisha wanatwaa ubingwa huo ambao mara ya mwisho kuutwaa ilikuwa ni msimu wa 2011/12.


Mkude alisema kuwa, wamejipanga kuhakikisha wanajituma kwa nguvu zote uwanjani ili wafanikiwe kupata ushindi katika michezo yote sita iliyobaki.


“Tunahitaji kushinda mechi zote zilizobakia ili kuweza kutimiza lengo letu kwani dhamira yetu ni ileile ya kutwaa ubingwa msimu huu, hivyo tunahitaji kuungana katika kipindi hiki cha mwisho kwa kuendelea kuimarisha umoja wetu kuanzia wachezaji, viongozi na mashabiki kwa ujumla,” alisema Mkude.


1 COMMENTS:

  1. Mkude na wachezaji wa Simba wahamasishe wachezaji wote wa Simba wajue kuichezea Simba ni fahali kubwa sana na mhakikishe mnabeba kombe la ligi kuu ya Tanzania nyinyi wachezaji mnapaswa kujivunia kama mtaipa Simba ubingwa ambao imeukosa mda mrefu pia kama wachezaji wa Simba thamani yenu itapanda mara dufu kwa wale mtakao kuwa mkiichezea Simba katika mashindano ya klabu bingwa ya Afrika nawatakia mema ili muweze kutawazwa mabingwa wapya wa 20 17 wa ligi kuu simba nguvu moja

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV