March 24, 2017

TAMBWE

Mashabiki mbalimbali wa Yanga, wameendelea na michango ili kupata nauli kuwasaidia wachezaji wao kwenda kutibiwa Afrika Kusini.

Mashabiki na wanachama hao wa Yanga, wanataka Donald Ngoma na Amissi Tambwe wanakwenda kutibiwa Sauz matibabu ya uhakika.

Washambilizi hao wawili wamekuwa majeruhi na kuipa Yanga wakati mgumu katika mechi zake muhimu.

Kupitia makundi mbalimbali ya Whatsapp, michango hiyo imekuwa ikiendelea ili kufanikisha lengo hilo.

1 COMMENTS:

  1. Mnahangaika kutibia vizee, wawambie umri wao halisi kwanza kabla hamjapoteza pesa zenu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV