March 24, 2017



Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, jana walikabidhiwa Kadi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Shirika Bima la Afya la Taifa (NHIF) kwa lengo la kuwasaidia kupata matibabu ya uhakika wanapokuwa wanaumwa.

Timu hiyo kwa sasa inajiandaa na michuano ya mataifa Afrika kwa vijana inayotarajia kufanyika nchini Gabon, Mei, mwaka huu.

Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Angela Mziray amesema kuwa lengo la kutoa kadi hizo kwa wachezaji hao ni kuwasaidia kupata matibabu kwa urahisi katika vituo vyote nchini hata wakiwa nje ya majukumu ya timu ya taifa.

“Kadi za Bima ya Afya ni zinatoa mfumo rahisi wa kuweza kupata matibabu na lengo la kufanya hivi ni kuweza kuwasaidia vijana hawa ambao ni matarajio ya kesho kwani hii siyo mara ya kwanza kufanya kazi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na sasa hivi tunatoa huduma katika vituo 6,500 nchini.

“Kiukweli hili siyo jambo dogo kwa vijana wetu maana linaleta hamasa na umuhimu mkubwa kutokana wao kuweza kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za Afya kwa kadi ambazo tunawapatia kwa sababu wao wanafanya mazoezi na wanaweza wakaumia hivyo zitawasaidia katika kupata huduma nzuri bila ya kutumia pesa yoyote kutoka mkononi mwao,” alisema Mziray.

Upande wa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema wanashukuru mfuko huo kutokana na mchango huo waliutoa kwa timu huyo huku akiwaomba wawe sehemu ya wadhamini wa timu hiyo inayojiandaa na fainali za Afrika nchini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic