March 13, 2017


Jose Mourinho tayari yuko London kuwavaa Chelsea katika mechi ya Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali, leo.

Lakini kikosi chake kitawakosa nyota wake muhimu kama Zlatan Ibrahimovic, Wayne Rooney, Anthony Martial na Marcus Rashford.

Bado hiyo haimzuii Mourinho kupanga kikosi bora na ifuatayo ni mifumo mitatu anayoweza kuitumia.

Moja: 





 Atamtumia Marouane Fellaini kama mshambulizi kuhakikisha mabeki wa Chelsea hawapandi.


Kawaida Fellaini si mshambulizi, lakini atafanya hivyo kuwachanganya mabeki wa Chelsea hasa kwenye vichwa na pia umiliki wa mpira ikiwa ni kama kuziba pengo la Zlatan.

Lakini hii ni kuwanyima raha na utulivu mabeki wa kati wa Chelsea, hasa David Luiz ambaye akitulia, anasaidia upangaji wa mashambulizi.



Mbili: 



Young ni kiungo lakini Mourinho anaweza kumchezesha kama mshambulizi sababu ya kazi yake na nyumba yake kukawa na Lingard na Mata ambao uchezaji wao ni kipaji zaidi. Lakini nyuma yaoakawa Mkhtaryan ambaye atakuwa akisaidia kupandisha mashambulizi.


Tatu: 

Mkhitaryan anaweza kuwa juu, huyu ana uwezo mkubwa wa kufunga, kumiliki mpira au kutoa pasi za za mwisho.

Pogba, Fellaini, Mata na Lingard wakawa nyuma yake na Man United ikatumia muda mwingi kuwa na mpira ili kupambana na Chelsea yenye kasi.

Lazima Man United washambulie sana ili kuizuia Chelsea kushambulia kwa kasi lakini lazima wawe makini na mashambulizi ya kushitukiza.

2 COMMENTS:

  1. Naona utabiri haukufaulu, anyway, nimependa hiyo creativity yako.

    ReplyDelete
  2. Zaidi ya hapo
    MARCUS RASHFORD alicheza pamoja na utabiri kwamba asingecheza.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic