March 13, 2017 Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki.

Stars inaweza kucheza na kati ya Zambia na Rwanda au timu nyingine kwa kuwa kumekuwa na taarifa tofauti.

Lakini kikosi cha Mayanga kiliongozwa na nahodha Mbwana Samatta anayekipiga nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk kina vijana wengi zaidi.

Makipa; 
Aishi Manula (Azam), Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Mabeki;
 Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Yanga), Mohammed Zimbwe ‘Tshabalala’ (Simba), Gardiel Michael (Azam), Andrew Vincent (Yanga), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).

Viungo;
 ni Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domayo (Azam), Muzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (DC Tennerife) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).


Washambuliaji;
Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden), Ibrahim Ajibu (Simba), Mbarak Yussuf (Kagera Sugar) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).

1 COMMENTS:

  1. Timu iliyotangazwa nzuri lakini nasikitika sana kuna baadhi ya wachezaji wako nje wanaocheza mpira wameachwa bila kuitwa sio kitu kizuri kabisa kwa maendeleo ya soka la Tanzania walioachwa ni Maguli na Danny Lyanga ná mdogo Zanako alionyesha uwezo mkubwa sana wote walitakiwa kuitwa mtu na mdogo wake uwezo wanao ukilinganisha na walioitwa hapa hayo ni maoni yangu kama mdau wa mpira.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV