March 16, 2017



Monaco ikiwa nyumbani imeitwanga Man City kwa mabao 3-1 na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ushindi wa Monaco unafanya mabao kuwa sare ya 6-6, lakini mabao ya ugenini yanaibeba Monaco ambayo ilifungwa 5-3 jijini Manchester katika mechi ya kwanza.

Monaco walipata mabao mawili ya haraka katika kipindi cha kwanza kupitia Mbappe Lottin na Fabinho, yakadumu hadi mapumziko.



Kipindi cha Leroy Sane aliamsha matumaini ya Man City kwa kufunga bao katika dakika ya 71 katika dakika ya 77, Tiomoue Bakayoko akayazima kwa kufunga bao la tatu kwa Monaco ambayo imesonga mbele na kumuacha Kocha Pep Guardiola wa Man City na majonzi rundo.


VIKOSI
Monaco: Subasic, Sidibe, Raggi, Jemerson, Mendy, Fabinho, Bakayoko, Lemar, Bernardo Silva, Germain, Mbappe-Lottin.
Subs: De Sanctis, Jorge, Dirar, Joao Moutinho, Irvin Cardona, Irvin Cardona, Diallo, Toure.


Man City: Caballero, Sagna, Stones, Clichy, Kolarov, Sane, Fernandinho, Silva, De Bruyne, Aguero, Sterling.
Subs: Bravo, Zabaleta, Jesus Navas, Delph, Otamendi, Toure, Iheanacho.
Referee: Gianluca Rocchi (Italy)






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic