March 15, 2017



Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) limezifungia Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

TRA kupitia Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart imewataka wafanyazi kuacha kila kitu cha shirikisho hilo ndani.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amethibitisha hilo na kusema TFF haikutimiza walichokubaliana kuhusiana na wanachowadai.


“Ni kweli tumezifunga na hiyo ni hatua ya mwisho kwetu kufanya hivyo. Tulikubaliana kulipa tunachowadai na muda umepita,” alisema.

Alipouliuzwa kuhusiana na kiasi: “Haya ni masuala ya sisi na wenyewe.”


Yono walihusika katika kuzifunga ofisi hizo na kuwataka wafanyakazi wote kutotoka nje ya ofisi na kuacha kilakitu ndani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic