March 22, 2017

HANS POPPE AKIWA NA AWESU

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude, amesema kuwa kama uongozi wa klabu hiyo una mpango wa kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Madini FC, Awesu Awesu, basi ufanye sasa kwa kuwa jamaa ni mashine.

Jumapili iliyopita, Awesu alionyesha uwezo mkubwa katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Simba iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na Simba kupata ushindi wa bao 1-0.

Kiwango cha mchezaji huyo kilimchanganya Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe na kujikuta akimtaka mchezaji huyo amtafute.
MKUDE

Mkude amesema kuwa mchezaji huyo ni mzuri na aliwavuruga sana katika sehemu ya kiungo licha ya kikosi chao kuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu.

“Anajua ni mchezaji mzuri anayejiamini kwani alijitahidi sana kufanya vizuri katika mechi hiyo na alikuwa haogopi.

“Kama uongozi wetu una mpango wa kutaka kumsajili, siyo mbaya kwani baadhi ya viongozi walimuona, hivyo wao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho lakini binafsi nilivutiwa na uwezo wake na ni vyema wakifanya hivyo sasa,” alisema Mkude.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV