March 12, 2017


Kiungo mwenye kasi wa Yanga, Simon Msuva anaamini Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri itakaposafiri kwenda Lusaka, Zambia kuivaa Zanaco, Jumamosi ijayo.

Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Zanaco katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Jambo ambalo linawapa hofu mashabiki wengi kwa kuwa Yanga ilikuwa nyumbani na sasa inaenda ugenini.

Lakini Msuva ambaye alikuwa tishio kwenye ngome ya ulinzi ya Zanaco, amesema wana nafasi.

“Tuna nafasi ya kujirekebisha, kikubwa mashabiki wasichoke kutuunga mkono.

“Mpira una mambo mengi, hivyo waamini lolote linawezekana na wawe pamoja na sisi,” alisema ambaye alifunga bao la Yanga wakati ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga, jana.

Tayari Zanaco wamesema, watalifanyia kazi suala la Msuva kuonekana ni tishio kwao ili asiwe na madhara katika mechi hiyo ya marudiano mjini Lusaka, Zambia.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV