March 12, 2017


Pamoja na kwamba kiungo Said Ndemla kukosa nafasi ya kwenda kujiunga na AFC ya Sweden, klabu hiyo bado itaendelea kumfuatilia.

Mmoja wa maofisa wa AFC, Frank Thomas amesema wanajua Ndemla bado ni kinda na ana nafasi ya kuendelea kufanya vizuri.

“Inawezekana ilikuwa ni suala la kutoelewana kati yetu (klabu). Lakini si jambo baya kwa kuwa ni majadiliano.

“Tutaendelea kumfuatilia Said na bado ana nafasi kwetu,” alisema kutoka Sweden.


AFC ndiyo timu anayochezea Mtanzania, Thomas Ulimwengu ambaye awali, aliwika akiwa na TP Mazembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV