March 14, 2017Beki wa pembeni wa zamani wa Simba, Emily Mugeta ameonyesha anaanza kuzoea na kupanda katika soka nchini Ujerumani baada ya kupata nafasi katika kikosi bora cha mwezi Februari.

Kikosi bora cha mwezi katika daraja la tano nchini Ujerumani huteuliwa kulingana na maksi ambazo mchezaji anapata kutokana na mechi nne au tano kila mwezi.


Mugeta kwa mara ya kwanza ameingia katika kikosi hicho akiwa beki wa kulia.


Akizungumza moja kwa moja kutoka nchini Ujerumani, Mugeta alisema ni mara ya kwanza na pia changamoto.

“Kama nimefikia hapo, inakuwa ni changamoto. Ningependa kuingia tena na tena na hizi ndiyo changamoto za kutaka kukua,” alisema beki huyo aliyekulia kisoka jijini Mwanza na baadaye timu ya vijana ya Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV