March 7, 2017Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma MWambusi amesema hawatafanya mzaha dhidi ya Kiluvya FC, lakini wanaona ratiba ni ngumu kwao.

Yanga inaivaa Kiluvya FC leo katika mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam HD.

"Unajua tunachotaka kufanya ni kuendelea kufanya vizuri lakini utaona ratiba yetu ni ngumu. Tunacheza mfululizo mechi za ligi na za kombe la shirikisho.

"Tunajua wamepanga TFF au Bodi ya Ligi, hatuwezi kuingilia. Tutakachofanya ni kueleza ukweli lakini tutacheza bila dharau. Tunataka kushinda," alisema.

Mara ya mwisho, Yanga ilikuwa uwanjani Jamhuri mjini Morogoro kuwavaa Mtibwa Sugar katika mechi iliyoisha kwa suluhu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV