March 14, 2017


Kikosi cha Simba chini ya Kocha Joseph Omog kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho.


Simba itashuka dimbani Jumapili kuwavaa Madini FC katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Jumapili.

Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema vijana wake wanaendelea vizuri.

“Mazoezi yanaendelea vizuri, hii ni kuonyesha tunaipa uzito mechi hiyo,” alisema.

Simba imekuwa ikiendelea na mazoezi kwenye viwanja vya  Burka Cofee Estates nje kidogo ya jiji hilo la Arusha.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV