March 14, 2017


Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali sasa ni mhitimu wa kidato cha nne, yaani "Form Four".

Baada ya kuhitimu, Dalali maarufu kama Triumph amekuwa akijigamba kuwa ni mtu mwingine na ana uwezo wa kugombea uongozi Simba au kupata kazi sehemu ambazo awali asingefanya hivyo.


"Dalali ana raha sana, unajua wakati ule alikatwa kwenye uchaguzi wakati akiwa mwenyekiti kwa kuwa kanuni zilikuwa zinaeleza lazima mgombea awe na elimu ya kidato cha nne na yeye ni darasa la saba.


"Baada ya hapo akaamua kurudi QT na sasa amehitimu, ukikutana naye muulize," kilieleza chanzo.

Alipotafutwa Dalali na kugusiwa kuhusiana na hili, akasema:


"Kweli nimetimu (kicheko), lakini si kweli kwamba nimekuwa nikijigamba (kicheko), unajua hao ni wajukuu zangu hivyo wamekuwa wananitania (kicheko).


Alipoulizwa kama atagombea Simba: "Hayo si ya sasa hivi kwanza. Lakini kikubwa nimehitimu kidato cha nne."1 COMMENTS:

  1. Trump( Rais wa
    America)na Triumph ni vitu viwili tofauti, waandishi kioo cha jamii tujitahidi, tusidhalilishe taaluma.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV