March 8, 2017Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kikosi chake hivi sasa kipo vizuri na tayari kwa ajili ya kuhakikisha kinafanya vizuri katika mechi zake zote zilizobakia bila ya kujali ni timu gani kitakayokutana nayo ikiwemo Simba.


Simba wanatarajiwa kuvaana na Kagera Machi 11, kwenye Uwanja wa Kaitaba, uwanja ambao umekuwa mgumu Simba kupata ushindi kwa kipindi kirefu.


Kocha huyo amesema tangu alipofanikiwa kumsajili mlinda mlango, Juma Kaseja mambo yamebadilika katika kikosi chake hicho ambapo hivi sasa kila mchezaji anataka mafanikio hivyo timu ya Simba inatakiwa kujipanga.

Maxime alisema wanataka kumaliza michuano ya ligi kuu wakiwa katika nafasi tatu za juu na amepanga kuitumia mechi dhidi ya Simba kutoka nafasi ya nne wanayoshika hivi sasa wakiwa na pointi 42 mpaka ya tatu ambayo inashikiliwa na Azam FC yenye pointi 44.

 “Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya mechi zetu za ligi kuu zilizobakia, lakini napenda kuchukua nafasi hii kusema kuwa timu zote tutakazokutana nazo katika kipindi hiki cha lala salama zinatakiwa kujipanga na hususani Simba ambayo tutakutana nayo hivi karibuni.


“Tunataka kuhakikisha tunamaliza ligi kuu tukiwa katika nafasi tatu za juu hivyo hatutaki mchezo kabisa,” alisema Maxime huku akiwapongeza wachezaji wake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV