March 2, 2017


Kocha Luis Enrique ameamua hatangeza mkataba wa kuendelea kuifundisha Barcelona.

Mkataba wake wa sasa unaisha Julai, mwaka huu ikiwa ni muda mchache baada ya kwisha kwa La Liga.

Rafiki wa karibu, amesema Enrique ameamua kutoongeza mkataba.


“Huu ni uamuzi wake, ameamua hivyo na utasikia baadaye atatangaza,” alisema rafiki yake wa karibu akizungumza na SALEHJEMBE moja kwa moja kutoka jijini Barcelona.

Kocha wa Sevilla, Jorge Sampaoli ni kati ya wanaopewa nafasi ya kuchukua nafasi yake.

Rafiki yake huyo amesema, Enique ameona anahitaji kuendelea na kazi hiyo bila ya presha kubwa kama aliyonayo sasa Barcelona aliyowahi kuichezea.

Hata hivyo amesema, bado hajawataarifu rasmi viongozi wa klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV