Na Dr Haroun Haroun
Yanga ina daktari wa timu anaitwa Dr Edward bavu nafikiria ana taaluma ya kutibia wachezaj vizuri, lakini wakati mwingine kwa sisi madaktari ikitokea ukishindwa kumtibu mgonjwa unaweza kuomba daktari mwenzio akusaidie.
Nilipigiwa simu na Mjumbe mmoja wa yanga ili nimsaidie kumtibu Donald Ngoma baada ya kutoka Zanzibar , Nilifanya hivyo nafikiria hii inatokana na weledi wangu mzuri wa uelewa katika taaluma ya matibabu ya michezo, nilimpokea nikamfanyia vipimo pamoja na matibabu (angalia picha na maelezo ya tiba hapo chini).
Nimewasaidia wachezaji wa yanga waliokuwa na shida mbalimbali za kimatibabu hasa yale yaliyokuwa sugu katika michezo (Hissan) wewe ni shahidi, nina reference ya Mwashiuya, Juma Abdul na Canavaro pamoja na wachezaj wengine mbalimbali sijawahi lalamikiwa hata siku moja.
Nilimtibu Kwa muda wa wiki mbili kwa jeraha la goti na kupona kabisa ,nakumbuka tarehe 3 Februari, Yanga walicheza dhidi ya Stand United nikiwa nyumbani naangalia mchezo huo ambao Ngoma aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo, baadaye nikamwandikia sms kwa Whatsap kujiridhisha kama bado jereha linamsumbua,? akasema, hapana anachoumwa Sasa ni groin ikiwa na maana kiuno au wengine hupenda kusema nyonga na alinijibu Kwa whatsap SMS (screen shot nimekutumia), nikamuahidi kumsaidia tena kwa tatizo hilo,baada ya matibabu akasema anajisikia amepona na hata majibu ya vipimo hayakuonyesha tatizo (picha za vipimo na matibabu hizo nimetuma).
Kitaalamu Kuna aina nne ya matibabu katika mpira, kuna sports medicine doctor, physiotherapy, sport nutrition advisor na chiropractor ambayo tunaita matibabu mkandamizo utaalam huu nchi yetu Hakuna, Ngoma aliwaongopea viongozi wa Yanga SC kwa kuja na report ya kutengenezwa kutoka London Health ambayo imeandikwa na physiotherapy na siyo daktari wa Michezo.
Fomu ya FIFA ina sehemu ya daktari wa timu na daktari wa viungo, daktari wa viungo hawez kuandika report Ya Mchezaji itakuwa mara ya kwanza Tanzania.
Ukitazama report ya London Health haiko kwenye maandishi ya kidaktari kabisa inaonekana ilikuwa mahitaji ya Mgonjwa, report ya Medical ina sehemu tatu, historia ya mgonjwa ,vipimo na ugonjwa ulioonekana na matibabu yaliyofanyika ambapo daktari wa mazoezi atachukua report kutoka Kwa daktari.
Niliwaambia ukweli viongozi wa Yanga SC na wewe ukiwemo uliponiuliza (Februari 18) juu ya tatizo lake, nikawajibu kuwa amepona na hana tatizo lolote kiafya hicho ndicho kilichomkasirisha Ngoma na kuamua kunichafua, ukweli ndio umenifanya mimi kuchafuliwa.
Sio kitu kizuri kuonyesha report ya Mgonjwa lakini hamna namna, nataka uma wa wana Yanga na wapenzi wa mpira waujue ukweli kuhusu Ngoma, Yanga SC wamekuwa wanaleta wagonjwa kwangu wakati wana daktari wa timu hii inaonyesha ubora wangu wa kazi na imani waliyonayo kwangu, sio jambo jema kwangu kulikalia kimya jambo ambalo linahatarisha mustakabali wa taaluma yangu.
Niwaombe radhi wote niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine, nawaomba mliokuwa na imani muendelee kuniamini na sitowaangusha, imani yenu kwangu isipotee kwa jambo hili.
Mimi naona huyu mchezaji hatufai yanga tunaonata mafanikio Leo unakuwa na mtu ambae hana uchungu na timu.Ngoma hajitumi uwanjani ukilinganisha na alivokuja yanga.Tumfungulie mlango wa kutokea,Tuna wachezaji wazawa wenye mchango mkubwa kwenye timu kama Msuva kuliko hata huyo ngoma.aende zake
ReplyDelete