Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amefunga mabao mawili na kuiwezesha Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana.
Samatta alifunga bao la kwanza katika dakika ya kwanza tu katika mechi hiyo ya kirafiki katika kalenda ya Fifa.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili Botswana nao walionyesha uhai lakini Stars walikuwa imara.
Mara kadhaa, kipa wa Botswana, alionyesha umahiri na kuokoa mikwaju kadhaa.
Samatta alishindilia bao la mwisho zikiwa zimebaki dakika chache akipiga mkwaju matata wa adhabu.
0 COMMENTS:
Post a Comment