March 11, 2017




Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba, leo wanacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dom iliyopo Ligi Daraja la Kwanza lakini wakali hao wa Msimbazi wamesema wala hawatadharau mchezo huo na wamepanga kushusha kikosi cha kwanza.

Ligi Kuu sasa hivi ipo kwenye mapumziko kupisha michuano ya Kombe la FA pamoja na michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga na Azam zinashiriki.


Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Ikumbukwe katika mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 ambapo ulipigwa uwanjani hapo Septemba 3, mwaka jana katika mechi iliyoandaliwa na uongozi wa chama cha soka mkoani humo. Mabao ya Simba yalifungwa na Abdi Banda na Said Ndemla.

Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja amesema wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mchezo huo na wanauchukulia kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la FA dhidi ya Madini FC ya Arusha utakaopigwa Machi 19, mwaka huu.


 “Tumejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo ambayo ni muhimu kwetu kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi yetu ya robo fainali ya Kombe FA, hivyo tutaingia uwanjani kwa ajili ya kupambana na kuhakikisha tunaibuka na ushindi.


“Lakini pia tunataka kuendeleza rekodi yetu ya kufanya vizuri mkoani hapa, tena dhidi ya Polisi Dodoma ambapo mwaka jana tuliifunga mabao 2-0 katika mchezo wetu wa kirafiki, hivyo nitumie nafasi hii kuwataka wapenzi na mashabiki wa timu zote mbili kujitokeza kwa wingi ili waje wapate burudani ya soka la kuvutia,” alisema Mayanja.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic