Straika wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, ametamka hadharani kwamba mashabiki wa timu hiyo hawatakiwi kukata tamaa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa sababu bado wana nafasi ya kupambania ubingwa huo kwenye mechi zijazo.
Straika huyo mwenye mabao saba, amesema kwamba wanatambua ugumu walionao baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Mbeya City lakini wana nafasi kubwa ya kurekebisha pale walipokosea kwenye michezo inayofuata.
Mavugo amesema kwamba bado wataendelea kupigania pointi zilizopo mbele yao kuifanya timu hiyo iweze kuchukua ubingwa kwa msimu huu ambao umekuwa ukitamaniwa na kila mmoja kwenye kikosi hicho.
“Hakuna kukata tamaa, tuna kila sababu ya kushinda mechi zijazo licha ya kupoteza mechi hii na Mbeya City kwa kupata pointi moja, lakini siyo mbaya na kikubwa tupiganie tu pointi zilizopo.
“Bado tuna nguvu ya kupambana na wengine na tunawaahidi kwamba tutalifanikisha suala hilo licha ya kuwa Yanga wao nao wanafanya vizuri kwenye mechi zao,” alisema Mavugo.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment