March 6, 2017



Nahodha na beki kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amezitaja mbinu tatu ambazo watazitumia katika harakati zao za kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Cannavaro amezitaja mbinu hizo kuwa ni ushirikiano, kujituma uwanjani na kuwa na nidhamu ya mchezo kwa kila mmoja wao wanapopambana na timu mbalimbali bila ya kujali ukubwa au udogo wake.

Beki huyo amebainisha hayo kabla ya mchezo wao wa jana Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo walikuwa wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 52, nyuma ya vinara Simba wenye pointi 55.

“Tutaendelea kupambana hadi mwisho kuona itakuwaje, hatuwezi kukata tamaa wala kujiona wapweke kutokana na kuzidiwa pointi na wapinzani wetu.

“Bado naamini tuna uwezo mkubwa tu wa kutetea taji letu kwa sababu nafasi ya kufanya hivyo tunayo, tena ni kubwa tu. Ili tufikie malengo hayo, ni lazima tuwe na ushirikiano baina yetu, tujitume uwanjani na kuwa na nidhamu ya mchezo bila ya kuonyesha dharau kwa timu yoyote ile tutakayokutana nayo,” alisema Cannavaro.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic