March 15, 2017



Toto Africans ya Mwanza, imesema kuwa, mechi yao dhidi ya Simba haina umuhimu kwa sasa licha ya kufahamu kwamba wapo kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo imesemwa na ofisa habari wa timu hiyo, Cathbert Japhet ambaye amebainisha kwamba wanachoangalia kwa sasa si mechi yao dhidi ya Simba bali ni kupata matokeo mazuri kwanza dhidi ya Majimaji na Yanga.


Toto inayoshika nafasi ya tatu kutoka chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 25, imebakiwa na michezo sita kabla ya kumalizika kwa msimu huu. Mechi hizo ni dhidi ya Majimaji, Yanga, Simba, JKT Ruvu, Azam na Mtibwa Sugar.

“Tunajua hatupo kwenye nafasi nzuri katika msimamo na tunaendelea kupambana kuhakikisha hatushuki daraja msimu huu, hivyo ni lazima kwanza kuzitolea macho mechi za karibuni na si za mbali.

“Tutacheza na Simba hapo baadaye, lakini kabla ya hapo, tutakuwa ugenini dhidi ya Majimaji na Yanga, hizo ndizo tunazoziangalia sana kwa sasa na si ile ya Simba kwani hiyo haina umuhimu zaidi ya hizi za karibuni.

“Bado hatujafikia malengo yetu tuliyojiwekea msimu huu, hivyo ni lazima tuendelee kujipanga kuhakikisha tunakuwepo tena katika ligi kwa msimu ujao,” alisema Japhet.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic