March 21, 2017
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wamepokea kwa mikono miwili sehemu ya ushindani mpya baada ya kusikia wamepangiwa MC Alger ya Algeria.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limeipangia Yanga kucheza na timu hiyo katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

“Tumeona kuhusiana na kupangwa na timu hiyo. Tumefika hatua hii tulitarajia kupangwa na timu yoyote.

“Hivyo hatuna sababu ya kusema tumeshituka sana, tunajua kuna ugumu na muhimu ni maandalizi ya kutosha,” alisema Mkwasa.


Katibu huyo ambaye kitaaluma ni kocha, alikiri Yanga imekuwa katika wakati mgumu kifedha lakini imekuwa ikijitahidi kufanya kila linalowezekana ili mambo yaende safi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV