March 2, 2017Viongozi wa Simba wamemuweka “mtukati” beki wao Juuko Murshid na kuhoji kilichosababisha achelewe bila ya taarifa.

Taarifa zinaeleza, pamoja na Juuko kurejea baada ya uongozi kumuomba kwa muda mrefu, bado viongozi walitaka kujua.

“Walikaa naye muda mrefu kidogo, walitaka kujua tatizo ni nini hasa. Maana alikuwa hana mawasiliano na uongozi na ilionekana kama alifanya makusudi.

“Uongozi unajua alifiwa na ulituma salamu za rambirambi, lakini yeye aliendelea kuwa kimya tu jambo ambalo liliwakera,” kilieleza chanzo cha uhakika.

Baada ya kutoka Afcon, Juuko aliomba kupumzika kwao Uganda ikiwa ni pamoja na kuomboleza kifo cha watoto wake mapacha watatu.

Lakini baada ya hapo alikuwa kimya bila ya kueleza jambo lolote.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV