Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji sasa inakwenda zaidi ya wiki tatu akiwa chini ya ulinzi.
Manji ni mgonjwa akiwa amelazwa katika hospitali ya Agakhan lakini ameendelea kuwa chini ya ulinzi.
Awali, alikuwa akilindwa na askari hadi saba wakati akiwa katika wodi ya Taasisi ya Moyo ya jakaya Kikwete iliyo katika Hospitali Kuu ya Muhimbili.
Lakini sasa Manji amelazwa Agakhan huku ulinzi ukiendelea.
Mmoja wa viongozi wa Yanga amesema wamekuwa wakienda kumuona akiwa amelazwa na wameambiwa yuko chini ya Idara ya Uhamiaji.
"Kweli bado yuko chini ya ulinzi, ingawa bado hatuelewi hasa nini kwa kweli. Ila tunajua yuko chini ya uhamiaji," alisema kiongozi huyo.
Awali Manji alituhumiwa kutumia madawa ya kulevya, akafikishwa mahakamani na kupata dhamana. Lakini baada ya kuachiwa ameshidwa na Idara ya Uhamiaji tena na bado haijatangazwa hasa ni nini.
Wahusika wengi wamekuwa wakikwepa kulizungumzia hilo na Manji anashikiliwa kwa lipi na kwa nini hajafikishwa mahakamani.
0 COMMENTS:
Post a Comment