March 21, 2017

SAMATTA AKIWASILI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (JNIA), USIKU HUU.

Mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ametua nchini tayari kujiunga na kikosi cha Taifa Stars.
Stars inajiandaa kucheza na Botswana katika mechi ya kirafiki itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

Baada ya mechi hiyo, Stars itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Burundi. Samatta ndiye ataongoza kikosi hicho akiwa nahodha.

MSEMAJI WA TFF, ALFRED LUCAS MAPUNDA (KULIA) AKIWA JNIA KUMPOKEA SAMATTA

Tayari kikosi cha Stars chini ya Kocha Salum Mayanga kimeanza mazoezi kujiandaa na mechi hizo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV