March 13, 2017
Chelsea haijawahi kufungwa na Man United tokea Oktoba, 2012.

Imecheza na Man United jumla ya mechi 11 bila ya kupoteza hata moja lakini timu hizo zinakutana leo.

Hata hivyo katika mechi za Kombe la FA, Man United wanaonekana kuwa wababe kwa kuwa wameshinda mara nyingi zaidi.

Man United wameshinda mara 8 dhidi ya mara 3 za Chelsea huku kukiwa na sare mbili.


Mabao ya kufunga, Man United ni zaidi kwa kuwa wamepachika 23 na Chelsea wana 11.

Man United inaivaa Chelsea katika mechi ya robo fainali ya FA Cup kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London, leo.


Tayari Man United wametua London kwa usafiri wa treni tayari kwa mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV