March 9, 2017Uongozi wa Yanga umemalizana na beki wake, Vicent Bossou kwa kumlipa mishahara yake.


Yanga waliingia kwenye mzozo na Bossou raia wa Togo ishu ikielezwa alikuwa anadai mishahara ya miezi minne.


Hata hivyo, baadaye Yanga ilifafanua kuwa alikuwa akidai mishahara ya miezi miwili baada ya kuwa amekwenda katika michuano ya Afcon huko Gabon.


Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kila kitu na Bossou kimemalizika.

"Bossou kama nilivyosema awali anatudai lakini sasa kila kitu kimekamilika, tumemlipa deni lake," alisema.


Awali Bossou, aligoma kuichezea Yanga kwa madai hayo ya kutolipwa mishahara yake, hali iliyosababisha aanze kuzozana na mashabiki mitandaoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV