March 9, 2017Mshambuliaji Donald Ngoma ameanza mazoezi katika kikosi cha Yanga.

Ngoma ameanza mazoezi baada ya siku kadhaa za kuidengulia timu hiyo kwa kisingizio cha kuumwa.

Hata hivyo, baadaye iligundulika ilikuwa ni janja, jambo ambalo liliwaudhi Wanayanga wengi.

Wakati Ngoma anaanza mazoezi, Amissi Tambwe ambaye alikuwa majeruhi na kufikia hadi kung’ang’ania kucheza, naye amerejea mazoezini.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema wachezaji hao tayari wameanza kujifua na wenzao.

“Tayari wako mazoezini lakini suala la kucheza Jumamosi kwa kweli sijui, au ni niseme wana asilimia chache sana,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV