March 16, 2017Kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, kinaondoka leo jioni kuifuata Zanaco kwao Zambia.

Yanga tayari wamewasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakisubiri kupaaa kwenda Lusaka, Zambia.
Mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya timu hizo ilipigwa jijini Dar es Salaam na kwisha kwa sare ya bao 1-1. Mechi ya Lusaka itapigwa Keshokutwa Jumamosi.


Kikosi kizima cha Yanga, wakiongozwa na Kocha George Lwandamina walitua uwanjani hapo saa 8 na nusu tayari kuanza maandalizi ya safari.


Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kila kitu kipo safi na wamejiandaa vizuri kwenye kupambana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV