March 1, 2017



Huku Yanga ikiwa imekiri kwamba beki wake, Vicent Bossou anadai mshahara wa miezi miwili na si minne kama alivyosema, taarifa nyingine zimeeleza, mgomo wake ni kutaka mkataba mpya na mnono.

Taarifa zinaeleza Bossou alishatangaza mgomo huo kwa watu wa karibu akiwemo beki Serge Wawa anayekipiga El Merreikh ya Sudan.

“Unajua Wawa ni rafiki wa Bossou, hivyo alishamweleza kuhusiana na hilo. Sasa Wawa ana urafiki na mmoja wa viongozi wetu, akamueleza hiyo hali,” kilieleza chanzo.

“Sisi tunajua Bossou anasema suala la mishahara lakini anajua cheki yake ilishaandikwa hata kabla hajarudi kutoka kwenye Afcon. 

“Lakini anafanya makusudi kwa lengo la kuongezewa mkataba mnono, jambo ambalo tunaona lisingefanikiwa kupitia migomo. Pia ujue bado kuna miezi kadhaa ili mkataba wake uishe.”


Bossou amekuwa akiendelea mazoezi na wenzake lakini hataki kucheza mechi kwa madai anadai mishahara ya miezi minne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic