Kocha Joseph Omog anaamini kama Simba itashinda mechi tatu za Kanda ya Ziwa basi itakuwa na nafasi nzuri ya kusema inaweza kubeba ubingwa.
Omog raia wa Cameroon amesema morali yao ipo juu lakini wanachotakiwa ni kuiendeleza na kushinda mechi hizo tatu mfululizo kwanza.
Lakini bado Yanga itatakiwa kushinda pia mechi nyingi dhidi ya Mbeya City na Omog amesema kila mechi itakuwa ngumu kwao.
"Lazima kushinda mfululizo ili kujihakikishia nafasi ya ubingwa. Yanga ilikuwa mechi ngumu na imepita, sasa ni vizuri kuangalia mbele," alisema.
Simba inaongoza Ligi Kuu Bara kwa kuwa na pointi 54 ikifuatiwa na Yanga wenye 49 lakini wana mchezo mmoja mkononi.
0 COMMENTS:
Post a Comment